• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Idara ya Maendeleo ya Jamii

MAENDELEO YA JAMII

UTANGULIZI:

MAENDELO YA JAMII NI NINI?

Maendeleo ya jamii ni mchakato wa kujenga uwezo wa jamii endelevu, inayojiamini na yenye uwezo wa kujituma na kushiriki kwa misingi ya usawa na kuheshimiana, katika kubaini mahitaji yao. Aidha kubuni, kuandaa, kutekeleza na kusimamia mipango ya kujiletea maendeleo kwa kutumia kikamilifu raslimali za ndani na nje.

Jamii hazifanani na hivyo matatizo ya jamii pia hutofanutiana.

Jamii hutofautiana kutokana na mila, imani, desturi, maadili na historia inayorithishwa kutoka kikazi kimoja hadi kingine na mazingira wanamoishi na kazi zinazowezesha kujikimu. Vigezo hivyo vinaweza kuwa vichocheo au vikwazo katika kuleta maendeleo.

USTAWI WA JAMII NI NINI?

Ustawi wa Jamii ni mchakato wa kujenga jamii kimaadili ili istawi kwa kumsaidia mtu mmoja mmoja mwenye tatizo la kifamilia ambalo linaweza kumsababishia madhara (kijamii, kisaikolojia na kiuchumi) au kikundi cha watu wenye tatizo linalofanana.

Ustawi wa Jamii unategemea zaidi uhiyari wa mhudumiwa na mtaalamu wa ustawi wa jamii kwa kumsaidia kufahamu tatizo alilonalo, kulikabili na kusikiliza ushauri na kuweza kuchukua uamuzi baada ya kushauriwa (kukabili tatizo). Pia mteja anatakiwa kutekeleza na kuyasimamia maamuzi yaliyofikiwa.

KAZI ZINAZOFANYWA:

MAENDELEO YA JAMII.

Kuunganisha nguvu za jamii na serikali ili kuondoa fikra tegemezi.

Kutoa elimu kwa vikundi vya kijamii na kiuchumi kwa njia ya kushiriki maonesho ya biashara na majadiliano.

Kufanya tafiti shirikishi za kijamii na kiuchumi ili kubaini fursa na vikwazo katika kujiletea maendeleo.

Kuimarisha demokrasia ili kuongeza kasi ya maendeleo ya watu.

Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango na miradi ya maendeleo.

Kuwezesha viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali kutengeneza ratiba za utekelezaji wa mpango/miradi endelevu ya maendeleo.

Kukusanya, kuchambua, kutafsiri na kutunza takwimu na kumbukumbu mbali mbali kwa ajili ya matumizi ya jamii/serikali na Halmashauri.

Kusimamia na kuratibu shughuli za maendeleo, jinsia na watoto.

Kuratibu masuala ya UKIMWI na athari zake katika jamii.

Kusimamia utekelezaji wa sera mbali mbali.

USTAWI WA JAMII.

Kutoa Huduma kwa Familia na watoto.

Kushughulikia masuala ya usuluhishi wa ndoa.

Kushughulikia matunzo ya mamba/watoto nje ya ndoa.

Kushughulikia matunzo ya mama/watoto katika wahalifu kwenye mahabusu ya watoto.

Kusimamia huduma kwa watoto sugu wanaokwenda shule ya maadilisho.

Kutoa huduma za marekebisho, utengamano na matunzo ya walemavu/wasiojiweza.

Kusimamia huduma za matunzo ya wazee nje na ndani ya makazi.

Kusimamia na kuratibu huduma za marekebisho ya walemavu.

Kusimamia na kuhimiza huduma za vituo vya kulelea watoto wadogo mchana.

Kushughulikia masuala ya watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi kwa kuhamasisha jamii waliyomo kuwaona kuwa ni watoto wao kupitia kamati husika.

SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA IDARA.

Uratibu wa mashirika yasiyo ya ki-serikali (NGO`s) na Asasi za kijamii (CBO`s).

Idara inajukumu la kuratibu shughuli za NGO`s na CBO`s na kusimamia utekelezaji wa sera ya Taifa ya NGO`s na CBO`s ya mwaka 2001 na sheria ya NGO`s Na. 24 ya mwaka 2002.

Aidha Idara inajishughulisha na yafuatayo:-

Kuelimisha jamii kuunda vikundi na umuhimu wa kuwa na katiba.

Kushauri na kusimamia uundaji wa katiba za vikundi.

Kuwezesha vikundi kupata elimu ya ujasiriamali.

Kusaidia vikundi kuandaa michakato ya miradi na mikakati ya biashara.

Kuratibu mfuko wa maendeleo ya wanawake ( W.D.F) na mfuko wa maendeleo ya vijana (Y.D.F) na kutoa mikopo yenye riba nafuu.

Mfuko unatoa mkopo kwa kikundi cha wanawake watono (5) na kuendelea.

Kikundi lazima kiwe na biashara na Akaunt ya Benki.

Kikundi lazima kitambulike katika ngazi ya kijiji na Kata.

Kikundi kiwe na mchanganuo wa mradi unaombewa mkopo.

Kikunndi kiwe na mdhamini

Wanakikundi wawe wanaishi katika kata husika.

Mkopo wa kuanzia ni Tsh 300,000 na ukirejeshwa unaongezewa 100% kwa mkopo unaofuata.

Mkopo unarejeshwa na riba ya 10%.

Mkopo unarejeshwa ndani ya miezi 6.

MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA (Y.D.F).

Jukumu kuu ya sehemu hii ni kuratibu utoaji wa mkopo hiyo kwa vijana katika Halmashauri.

Mikopo hiyo hutolewa na SACCOS baada ya kupata fedha za ruzuku kupitia Halmashauri.

Aidha masharti ya mikopo hiyo husimamiwa na SACCOS husika.

.Lengo kuu la Umoja huu ni kufanya kazi na jamii katika utumiaji wa raslimali zinazopatikana katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete Shughuli kuu zinazofanywa na umoja huu ni:-

Kutoa mafunzo ya stadi za ujasilia mali na usimamizi wa biashara.

Kutoa mafunzo ya stadi za maisha kwa watoto wa kike mashuleni na nje ya shule.

Kuratibu na kushirikiana na wadau katika shughuli za kudhibiti UKIMWI na athari zake katika jamii.

Jukumu kuu ni kushirikiana na wadau katika Halmashauri ili kuongeza uchangiaji wa mawazo, nyenzo, usimamizi, uratibu na utekelezaji wa afua za UKIMWI.

Kutumia kila jitihada katika kupunguza kiwango cha maambukizi mapya na kushughulikia athari zake.

Kuratibu shughuli za watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi ( MVC). Lengo ni:-

Kuwatambua watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika Halmashauri.

Kuunda kamati za MVC za vijiji na mitaa.

Kushirikiana na wadau katika kuwahudumia watoto kwa kuzingatia mahitaji yao.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI. October 24, 2020
  • FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 18, 2020
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 18, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Uzinduzi wa kliniki ya utoaji huduma kwa watoto wenye tatizo la miguu kifundo

    September 03, 2020
  • Taarifa ya vikao vya kisheria katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete

    February 25, 2020
  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019

    October 08, 2019
  • MWENGE WA UHURU MAKETE 2019

    September 19, 2019
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • KITULO FM BLOG
  • BEMIS
  • FFARS
  • HIMS
  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • FFARS
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@2016. Haki zote zimehifadhiwa