• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DED MAKUFWE AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA WAZAZI WOTE AMBAO WAMESHINDWA KUWAPELEKA WATOTO SHULE

Tarehe Iliyowekwa: January 16th, 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. William M. Makufwe leo Januari 16,2024, amekagua Uandikishaji wa wanafunzi, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi kupitia KAMAKA, katika kata mbili za Isaplano na Kitulo zilizopo Wilayani Makete.

Akiwa katika ziara hiyo, Ndg. William M. Makufwe, amewataka viongozi wote kuanzia ngazi ya Kijiji kuhakikisha kuwa wanasimamia zoezi la kiwabaini wazazi ambao hadi sasa Watoto wao hawajapelekwa Shule kwa mujibu wa sheria, kwakuwa kila mtoto ambaye amekidhi vigezo ana haki ya Kusoma.

"Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa akitoa Fedha nyingi sana kwaajili ya kuboresha miundombinu ya Elimu hapa Makete, sasa nashangaa kuona baadhi ya wazazi hawataki kuwapeleka watoto Shule, huu ni Ukatili, wachukulieni hatua za kisheria kwakuwa Elimu kwa mtoto ni lazima" Amesema Ndg. Makufwe.

Aidha, Ndg. Makufwe, amewataka watumishi wa Umma, kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba wananchi, ikiwa ni pamoja na kuwahimiza wanamakete kupambana na Udumavu, kutokana uelewa finyu wa matumizi ya Lishe bora Kwa watoto wenye umri chini ya Miaka 2. 

Naye Afisa Lishe, kutoka Hospitali ya Wilaya ya Makete, Bi. Agnes Columbani, amewataka wanamakete kuzingatia mlo kamili kwa Watoto wao, tangu akiwa tumboni kwa mama, ili kupambana na Udumavu.

"hakikisheni vyakula wanavyotumia watoto wenu vimezingatia makundi yote ya Chakula, kama vile protini, Wanga, madini ya chuma, pamoja kuzingatia upandaji wa miti ya Matunda, pamoja na Bustani za Mbogamboga kwenye Taasisi za Shule " Alisema Bi. Agnes Columbani.

Kwa Upande wake, Afisa Mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. Bwire Muyengi, amewataka wakuu wa Taasisi zote za Serikali, kuhakikisha kuwa makusanyo yote kuanzia ngazi ya kijiji yanawekwa Benki, ili kuwe na utaratibu katika utoaji, pamoja na kutumia mfumo katika matumizi yeyote yale.


Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.