• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YAANZA KAMPENI YA KUTOKOMEZA UDUMAVU

Tarehe Iliyowekwa: November 20th, 2023

Wakazi wa Kijiji cha Misiwa, kilichopo Kata Ukwama, pamoja na Kijiji cha Maliwa, kilichopo Kata ya Ipepo, Wilayani Makete, Mkoani Njombe, wametakiwa kuzingatia Vyakula vyenye Lishe bora, kwa kuwapa watoto wao makundi yote ya chakula ili kutokomeza Udumavu Wilayani humo.

Afisa Lishe wa Wilaya ya Makete Bi. Jackline Nannauka, amesema hayo leo Novemba 20, wakati akiongea na wakazi wa Vijiji hivyo, akiwa kwenye mkutano wa hadhara, wenye lengo la kutoa Elimu ya Lishe bora, ikiwa ni pamoja na kusisitiza ulimaji wa bustani za Mboga mboga kwenye sehemu za huduma za Kijamii kama vile Shule za Msingi na Sekondari.

"wanawake zingatieni Lishe bora kwa Watoto wenu, mtoto hatakiwi kulishwa chakula chochote kabla ya miezi sita kutimia, pia akinamama hakikisheni mnawahi Kliniki baada ya kuhisi mna ujauzito ili muweze kupewa elimu ya makuzi ya Mtoto tangu akiwa tumboni kwa Mama" Alisema Bi. Jackline Nannauka.

Kwa upande Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Makete, Bi. Esther Lamosai, akitoa Elimu ya ukatili wa kijinsia Kwa Watoto wadogo, amewataka wakazi wa Vijiji vya Misiwa na Maliwa, kuhakikisha kuwa wanakomesha tabia hizo ambazo zimeonekana kushamiri katika miaka ya hivi karibuni wilayani Makete.

"Chukue hatua kali za kisheria pale mnapogundua kumetokea unyanyasaji wa kijinsia wa watoto wadogo, pia ni aibu familia kumpeleka mtoto akafanye kazi za ndani, anahitaji kupata Elimu Bora , Lishe bora Ili aje awakomboe maishani" Alisema Bi. Esther Lamosai.

Naye, Bi. Erica Kabelege, akitoa Elimu ya Umuhimu wa Upimaji VVU, amewataka vijana pamoja na wenza wao kuwa na tabia ya kujipima ili waweze kutambua Afya zao, ikiwa ni pamoja na kuwakinga Watoto ambao watazaliwa, pamoja na kuzingatia Lishe bora katika makuzi yao.

"Pimeni Afya zenu, ikiwa ni pamoja na kuzingatia usafi baada ya kushiriki tendo la ndoa na mume au mke wako, ili muweze kumkinga mtoto na maambukizi ya Magonjwa, sambamba na kuhakikisha kuwa mtoto hapati Udumavu kwa kukosa Lishe bora" Alisema B. Ericka Kabelege.

Nao baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Misiwa, akiwemo Ndg. Atilio Ilomo, amewataka wanakijiji wenzake kuhakikisha kuwa wanaweka ratiba nzuri ya ulaji wa Vyakula bora, pamoja na na kuwapa nafasi akinamama wawalee Watoto wadogo vizuri Kwa kuwapunguzia majukumu yao kiuchumi.

Akihitimisha Mkutano huo wa Hadhara, Diwani wa Kata ya Ukwama, Mhe. Emmanuel Smith Sanga, amewataka wakazi wa Kata ya Ukwama, kuhakikisha kuwa kila mtu anajali Afya ya mwenzake kwakutoambukizana VVU kwa makusudi.

Ikumbukwe kuwa, Halamshauri ya Wilaya ya Makete, Leo Novemba 20, 2023, imeanza Kampeni ya Kutokomeza Udumavu wilayani hapa kwa kutembelea kata nne za Ipelele, Iniho, Ikuwo na Ipepo ili kuhakikisha kuwa kila mzazi anazingatia Lishe bora, kwa watoto waliopo chini ya miaka mitano.

Imeandaliwa na:

Kitengo cha mawasiliano Serikalini.

Halmashauri ya Wilaya ya Makete.







 

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.