• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

JUKWAA LA USTAWI WA MTOTO WILAYANI MAKETE LAGAWA VIFAA VYA SHULE KWA WATOTO WENYE UHITAJI

Tarehe Iliyowekwa: January 30th, 2024

Jukwaa la Ustawi wa Mtoto la Wilaya ya Makete, leo Januari 30, 2024, limetembelea kata ya Ipepo kwa ajili ya kutoa elimu ya malezi kwa wototo na kuwakabidhi vifaa vya shule wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.

Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya Kamati ya Maendeleo ya Kata (KAMAKA) ya Kata ya Ipepo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Makete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, amesema vifaa hivyo vimetokana na michango ya wadau mbalimbali wa ndani na nje ya Makete ili kuwashika mkono watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Aidha Ndg. Makufwe ameongeza kuwa, ukimnyima mtoto elimu leo, utakuwa umemfanyia Ukatili kwa kumtengezea mazingira magumu hapo baadae, na kumfanya kuwa tegemezi katika maisha yake yote, sambamba na kuharibu nguvu kazi ya Taifa la Tanzania.

Sambamba na hayo, Makufwe amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kutumia vifaa hivyo walivyokabidhiwa, katika kuboresha taaluma yao kwa kufaulu vizuri darasani, kwani serikali ya awamu ya sita imeboresha na inaendelea kuboresha miundombinu ya shule Wilayani Makete.

Kwa Upande wake, Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi, Maliwa, Ndg. Thomas Mwamalekela, amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ndg. William Makufwe, kwa kufanya jambo hilo, ambalo linawafundisha na kuwakumbusha kuwasaidia watu wenye mahitaji muhimu, hasa watoto.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliopata mahitaji hayo, Mtoto Ostela Sanga ameshukuru na kuahidi kuendelea kufanya vizuri katika masomo na kwamba vifaa hivyo vimeleta hamasa zaidi ya kusoma kwa bidii.

Ikumbukwe kuwa, Jukwaa la Ustawi wa Mtoto linaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Makete, ambapo leo limezindua zoezi la kutoa elimu ya malezi na kugawa vifaa vya shule katika kata ya Ipepo ambapo na kwamba zoezi hilo ni endelevu katika Wilaya yote ya Makete.


Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.