• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA NISHATI NA MADINI YAFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MRADI WA UMEME WA REA WILAYANI MAKETE

Tarehe Iliyowekwa: March 17th, 2025

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Dkt. David Mathayo David, akiambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), leo Machi 17, 2025, imeendelea na ziara yake mkoani Njombe kwa kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme katika Kijiji cha Mang’oto, Kata ya Mang’oto Wilayani Makete.

Akizungumza mbele ya Wakazi wa Kijiji cha Mang’oto, Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Dkt. David Mathayo David, amepongeza REA kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kusambaza umeme vijijini, huku akitoa wito kwa mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi ili kuhakikisha maeneo yote yaliyopangwa yanafikiwa kwa wakati.

Naye, Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Judith Salvio Kapinga, amewataka wakazi wa Wilaya ya Makete, kuendelea kuiamini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutokana na kuwa na mafanikio makubwa katika utekelezaji mkubwa wa Miradi yenye tija kwa wananchi hasa usambazaji wa Umeme wa vijiji kupitia REA.

 “Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kila kijiji kila kitongoji kinapata umeme, hapa wilaya ya Makete kimebaki kijiji kimoja cha Kigulu, ambapo tayari Suma JKT wanaenda kufanya kazi ya kuhakikisha kuwa umeme unapatikana katika kijijji hicho, hivyo tuendelee kumuunga mkono Rais wetu ili kazi hizi ziweze kukamilika na wananchi waweze kupata huduma bora”, alisema Mhe. Judith Kapinga.  

Kwa Upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, akiwemo Mbunge wa Jimbo la Busanda, Mhandisi Tumaini Magesa, amesema kuwa changamoto zote ambazo wananchi wamezisema mbele ya kamati hiyo, zitaenda kufanyiwa kazi kwakuwa serikali inyaoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu na inawajali wananchi wake kwa kiasi kikubwa.  

Naye Mkurugenzi wa REA, Mhandisi Jones Olotu, amesema kuwa, Serikali imejipanga kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme vijijini, ambapo katika siku za hivi karibuni wanatarajia kutangaza tenda nyingine ili kuongeza nguvu katika utekelezaji wa miradi hiyo hapa nchini.

Pia, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Ndg. Clemence Mwawite Ngajilo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuinyanyua Wilaya ya Makete kiuchumi, pamoja na watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wasikivu kwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili kuwaletea maendeleo.

Hata hivyo, Mkazi wa Mang'oto, Bw. Daniel Mbilinyi, ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea Umeme, kwakuwa umekuwa na tija kubwa kwa kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yao, hususan katika shughuli za uzalishaji na biashara.

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.