• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

KAMATI YA FEDHA MIPANGO NA UTAWALA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE

Tarehe Iliyowekwa: February 11th, 2025

Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala ya Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Februari 11,2025, imehitimisha ziara ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo katika Halmashauri hiyo, ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza kwa ziara hiyo hapo jana Februari 10,2025. 

Akizungumza mara baada ya Ukaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, na Diwani wa Kata ya Iniho, Mhe. Christopher Yonam Fungo, amesema kuwa, ziara hiyo imekuwa na tija katika kufahamu utekelezaji wa miradi pamoja na kujua changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakumba wasimamizi wa miradi  pamoja na wajenzi.

Sambamna na hayo, Mhe. Fungo, amewataka wananchi na wasimamizi wa miradi hiyo kukamilisha miradi hiyo kwa wakati na kutumia fedha za miradi hiyo kwenye jukumu lililokusudiwa ili iweze kuanza kutumika na jamii kutokana na umuhimu wake kwa wakazi wa maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Makete.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mhe. Hawa Kader, amesisitiza usafi kwenye miundombinu inayaojengwa kwenye maeneo yao hasa upande wa Elimu na Afya, kutokana na umuhimu wake kwa jamii.

Kwa Upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala, ambaye pia Diwani wa Kata ya Lupalilo, Mhe. Imani Mahenge, akiwa katika ziara hiyo, amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali ili miradi hiyo ikamilike kwa haraka kutokana na uhitaji wake hususani kwenye utoaji wa huduma za Afya.

Pia, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashari ya Wilaya ya Makete, Ndg. Jerry Daimon Mwaga, amesema kuwa, wao kama watendaji wa serikali wamepokea ushauri wa kamati hiyo, na kwamba watahakikisha kuwa unafuatwa ipasavyo ili miradi hiyo iwe na tija kwa wananchi.

Ikumbukwe kuwa, Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala, imekagua na Kutembelea Miradi 8 katika kata Saba ambazo ni Lupalilo, Tandala, Mbalatse, Lupila, Bulongwa, Kipagalo na Luwumbu, yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 3,018,879,296, pamoja na vikundi viwili vya Wanawake wanufaika na mikopo ya silimia 10 ambavyo vimekopeshwa kiasi cha shilingi  milioni 20,507,400.00.

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA - UTOLEWAJI WA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI 2025-2026 November 16, 2025
  • MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 September 01, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA AAGIZA KUKAMILISHA MIRADI KWA HARAKA

    November 26, 2025
  • MKURUGENZI MTENDAJI MAKETE DC , JERRY MWAGA, AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII

    November 13, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MAKETE MHE. KISSA KASONGWA AWATAKA WAFANYABISHARA WILAYANI HUMO KUWEKEZA NYUMBANI

    November 12, 2025
  • DED MWAGA AONGOZANA NA MENEJA TARURA KUKAGUA BARABARA YA MANG'OTO IBAGA

    November 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.