• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

LIMENI BUSTANI ZA MBOGAMBOGA , KUPAMBANA NA UDUMAVU- BI. JACKLINE NANNAUKA

Tarehe Iliyowekwa: November 24th, 2023

Kampeni ya Utolewaji wa Elimu ya Umuhimu wa Lishe Bora, kwa watoto wadogo imeendelea leo Novemba 24, 2023, katika kijiji cha Ihela, kilichopo kata ya Tandala, na kijiji cha Maleutsi, kilichopo kata ya Iwawa, ambapo wazazi na walezi wametakiwa kuhakikisha kuwa milo mitatu yenye mchanganyiko wa vyakula tofauti inapatikana majumbani mwao.

Akizungumza katika Kampeni ya kutokomeza Udumavu, Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Bi. Jackline Nannauka, amewataka wakazi wa vijiji hivyo, kuhakikisha kuwa wanawapa watoto wao, vyakula vyenye Protini kwa wingi kama vile Mayai, Nyama na mbogamboga ili waweze kuwa na Afya bora makuzi yao ya kila siku.

Aidha, Bi. Jackline Nannauka, ameongeza kwa kuwataka wananchi hao, kuhakikisha kuwa wanalima bustani za mboga mboga majumbani pamoja na maeneo ya shule kwa kuzingatia wingi wa wanafunzi, ili kila mtoto aweze kupata chakula bora ambacho kitamjenga kiakili.

Kwa Upande wake, Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Bi. Esther Lamosai, amewataka wakazi wa vijiji vya Ihela na Maleutsi, kuhakikisha kuwa wanapambana na ukatili wa kijinsia, kwa kutenga muda wa kuongea na watoto wao ili waweze kujua mienendo ya kitabia.

“Acheni kuwaozesha watoto wadogo, ni kosa kisheria, waacheni watimize ndoto zao, kila mzazi au mlezi atawajibika kwa kumkosesha Elimu mtoto wa kike“Alisema Bi. Esther Lamosai.

Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Ihela kilichopo kata ya Tandala, wilayani Makete, wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye Kampeni hiyo, wamekiri kuwepo kwa vyakula bora katika maeneo yao licha kuonekana kushamiri kwa utapiamlo, ambapo wamebainisha kuwa changamoto iliyopo ni namna bora ya matumizi ya vyakula hivyo.

Sambamba na hayo, Mchg, Festo Anderson Mbilinyi, wa KKKT, Usharika wa Ihela, cameshukuru kutolewa kwa Elimu hiyo muhimu ya  makuzi ya mtoto, kutokana na kuwepo kwa ongezeko la Utapiamlo, na kwamba kampeni hiyo itakuwa chachu kwa wakazi wa kijij hicho katika kupambana na Udumavu.

Imeatolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini. 

Halmashauri ya Wilaya ya Makete.

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.