• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE, WAWASILISHA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KATIKA KATA KWA ROBO YA PILI

Tarehe Iliyowekwa: February 15th, 2024

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya WIilaya ya Makete, leo Februari 15, 2024, limekaa kikao cha Robo ya Pili cha kujadili taarifa mbalimbali za Utekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Kata 23, zilizopo katika halmashauri, ikiwa ni mwaka wa fedha wa 2023-2024.

Akizungumza katika kikao hicho mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mhe. Christopher Fungo, amesema kuwa lengo la kikao ni kujadili taarifa za maendeleo ya miradi, na kwamba changamoto kubwa ya ubovu wa barabara ndani ya kata hizo  zimepelekwa kwa mamlaka husika ambao ni TARURA ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.

“ubovu mkubwa wa barabara zetu umepelekea kukosa mapato kwa kiasi kikubwa, hivyo changamoto hii imewasilishwa kwa mamlaka husika, na nyinyi madiwani mna nafasi ya kuwafuata hawa watu ili muweze kuongea kwa kina namna bora ya uboreshaji wa barabara katika kata zenu” Alisema Mhe. Fungo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. William M. Makufwe, amesema kuwa mpango wa halmashauri ni kuhakikisha zile barabara muhimu zote zinaingizwa TANROAD, ili ziweze kutengewa bajeti kubwa ambayo itarahihisha usafiri pamoja na ukusanyaji wa mapato, tofauti na bajeti za TARURA. 

Sambamba na hayo, Ndg. Makufwe, amesema kuwa, kutofanyika kwa vikao vya kisheria katika mji mdogo wa Iwawa uliopo halmashauri ya Wilaya ya Makete, ni kutokana na ufinyu wa mapato katika halmashauri hiyo sambamba na muingiliano wa majukumu yaliyo nje ya bajeti na kupelekea kupungua kwa mapato.

Nao baadhi ya Madiwani, wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, wameiomba TARURA, kuhakikisha kuwa wanaboresha barabara zote zilizopo katika halmashauri hiyo ili mapato yaweze kupatikana, na kuboresha huduma za wananchi katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kuziomba baadhi ya barabara kuingia kwenye mamlaka za TANROAD.

Ikumbukwe kuwa, kikao cha Baraza la Madiwani, cha kupitia na Kujadili taarifa za Miradi ya Maendeleo ya Kata, hufanyika kila baada ya robo kukamilika, ili kujadili namna Bora ya Utekelezaji wa Miradi hiyo.

Imeandaliwa na:

Kitengo cha Mawasiliano, 

Halmashauri ya Wilaya ya Makete.

 












Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA - UTOLEWAJI WA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI 2025-2026 November 16, 2025
  • MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 September 01, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA AAGIZA KUKAMILISHA MIRADI KWA HARAKA

    November 26, 2025
  • MKURUGENZI MTENDAJI MAKETE DC , JERRY MWAGA, AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII

    November 13, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MAKETE MHE. KISSA KASONGWA AWATAKA WAFANYABISHARA WILAYANI HUMO KUWEKEZA NYUMBANI

    November 12, 2025
  • DED MWAGA AONGOZANA NA MENEJA TARURA KUKAGUA BARABARA YA MANG'OTO IBAGA

    November 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.