• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MAKETE IPO TAYARI KWA BBT

Tarehe Iliyowekwa: May 26th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa, amewataka vijana na wanawake wa Wilaya hiyo kuchangamkia fursa ya uwepo wa Mradi mkubwa wa Kilimo wa BBT, “Building Better Tomorrow”, kutokana na umuhimu wake katika kujenga uchumi wa nchi pamoja na wakazi wa eneo hilo kiujumla.

Mhe, Kasongwa amesema hayo, Mei 26,2025, akiwa kwenye mkutano wa Hadhara na wakazi wa Kata ya Kinyika katika kijiji cha Nungu, mara baada ya kukagua Shamba ambalo litatumika katika Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora, BBT, kwa wakazi wa eneo hilo, na kubainisha kuwa BBT itaenda kubadilisha uchumi wa wanamakete pamoja na taifa nzima kwa ujumla.

“Niipongeze sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Menejimenti ya Wizara ya Kilimo kwa kuanzisha BBT ambayo imekuwa mkombozi kwa vijana wengi, sambamba na kufanya ukaguzi na kutoa elimu kwa Wananchi juu ya malengo ya BBT, ambapo Programu hiyo itakwenda kuwa chachu ya mabadilikoya kiuchumi” alisema Mhe. Kasongwa.

Aidha Mhe. Kissa, ameongeza kuwa, kupitia BBT, Makete itakwenda kuzalisha mazao yenye tija kwa kuwa kuna rasilimali watu ya kutosha na kwamba wanaenda kuanzisha kilimo Biashara ili kutimiza adhima ya maono ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo ya kuchangia asilimia 10 kupitia sekta hiyo muhimu ifikapo mwaka 2030 kupitia Agenda 10/30.

Kwa upande wake, Mhandisi Anitha James kutoka Wizara ya Kilimo, amesema kuwa Programu hiyo itakwenda kuchochea uzalishaji wenye tija na kupatikana kwa masoko ya uhakika kwa vijana na wanawake watakaonufaika na Programu hiyo ya BBT, na ametoa rai kwa Wanachi wa wilaya ya Makete ambao ni vijana na Wanawake kuchangamkia fursa hiyo ambayo itakwenda kubadilisha maisha yao.

Akizungumza kwa niaba ya wanananchi wa kijiji cha Nungu, Mwenyeketi wa kijiji hicho Bw. Essau Ndaga ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Programu ya BBT, ambapo itakwenda kuchochea maendeleo katika sekta ya Kilimo na kama kijiji kitatoa ushirikiano kwa waratibu wa Programu hiyo ili iwakomboe vijana na wanawake watakao kuwa wanufaika na Programu hiyo.

Ikumbukwe kuwa, Ukaguzi wa shamba na utoaji wa Elimu juu ya Programu hiyo kwa Wananchi umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Kissa Kasongwa pamoja na Mhandisi Anitha James ambaye ni Mratibu wa BBT ngazi ya Halmashauri kutoka Wizara ya Kilimo, ambapo ukaguzi huo umefanyika katika Kijiji cha Nungu Kata ya Kinyika Tarafa ya Matamba Wilaya ya Makete, ambapo zaidi ya Ekari 100 zimekaguliwa kwa ajili ya Kilimo cha Mahindi,Viazi,Ngano na Maharagwe kwa Vijana na wanawake wa Wilaya ya hiyo.

BBT, Jenga Kesho iliyo Bora, ni programu maalumu ambayo imeanzishwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo, ikiwa na lengo la kuongeza ushiriki wa vijana katika kilimo kwa kuwapatia mafunzo, maeneo ya mashamba, mitaji na kuwaunganisha na fursa za masoko.

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MAKETE IPO TAYARI KWA BBT

    May 26, 2025
  • WENYEVITI WA VIJIJI NA VITONGOJI WILAYANI MAKETE WATAKIWA KUFUATA ASHERIA, KANUNI NA MAADILI YA KAZI

    May 15, 2025
  • KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA NDG. ISAMAIL ALLI USSI ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI WILAYANI MAKETE

    May 06, 2025
  • WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VYOMBO VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA KANUZI ZA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.