• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MGOGORO WA ARDHI WATATULIWA

Tarehe Iliyowekwa: May 28th, 2022

Viongozi wa Wilaya ya Wanging'ombe na Makete kwa kushirikiana na Maofisa Ardhi wa Wilaya hizo na Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Njombe wamefanikiwa kuutatua mgogoro wa ardhi eneo la Kijiji cha Mang'oto na Makangalawe Wilayani Makete lililokuwa likigombewa na wananchi wa Kijiji cha Moronga kata ya Kipengere wilayani Wanging'ombe.

Eneo lililokuwa likizozaniwa ni ardhi iliyopo katikati ya Mto Lumemo na Matwaki

Wakati wa Utatuzi wa mgogoro huo, Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda, Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mh. Lauteri Kanoni, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Bi. Mariamu Mhaji, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ndg. William Makufwe wameshuhudia maafisa ardhi wakieleza GN zinazoonyesha mipaka ambazo zimetoa ufumbuzi wa mgogoro huo uliowapa uhalali wa umiliki wa eneo hilo wananchi wa vijiji vya Makete.

Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mh. Kanoni amewataka wananchi wa kijiji cha Moronga kata ya kipengele kuwa watulivu na kwa kuwa wamekubali matokeo ya mgogoro huo waishi kwa amani na upendo na majirani zao wa vijiji vya Makete.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amewataka wananchi wa pande zote mbili kufuata sheria, kanuni na taratibu wanapotaka kutumia ardhi ya Makete au ya Wanging'ombe bila kusababisha mgogoro wowote.

Wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili wamepongeza zoezi hilo la Utatuzi wa mgogoro na kuwasihi mawakala wa mapato kuendelea kusimamia Mapato kwenye eneo hilo la mpaka kati ya Makete na Wanging'ombe ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Makete imeweka geti eneo hilo ili kulinda na kukusanya mapato.

Wananchi na viongozi wa vijiji vyote akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Moronga Wanging’ombe Ndg. Romanus Mgaya wameridhia uamuzi uliotolewa na Serikali, huku kupongeza jitihada za Serikali katika kuutatua mgogoro huo kwa haki na amani bila upendeleo.

Mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na kufanya shughuli za uzalishaji mali kudorora kwa wananchi Vijiji kutoka pande zote za Wilaya ya Makete na Wanging'ombe.

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.