• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MHE. MKUCHIKA AHIMIZA KULINDA MILA NA DESTURI ZA KITANZANIA

Tarehe Iliyowekwa: August 27th, 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. Kapt Mstaafu George Mkuchika ameiasa jamii kuenzi mila na desturi za Tanzania ambazo ndio utambulisho wa Taifa hilo ndani na nje ya nchi, na kuacha kuiga utamaduni usiofaa wa Mataifa mengine.

Mhe. Mkuchika amesema hayo Agosti 27, 2023 Mkoani Njombe, wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufunga Tamasha la pili la Utamaduni lililokua na Kauli Mbiu "Utamaduni ni Msingi wa Maadili Tuulinde na Kuendeleza"

"Nawapongeza kwa kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambayo yanaenzi maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1962 alipozindua Wizara ya Vijana na Utamaduni ambapo alisema Taifa lisilokua na Utamaduni wake ni Taifa Mfu na ni sawa na mwili bila nguo" Mhe. Kapt Mstaafu George Mkuchika

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema, lengo la Tamasha hilo ni kutoa fursa kwa Watanzania kuufahamu Utamaduni wa Tanzania kuusherehekea, kuutunza, na kuuendeleza utamaduni wao pamoja na kubadilishana utamaduni wa mkoa mmoja na mwingine.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema katika Tamasha hilo, shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo shindano la kuibua vipaji la Njombe Vibe, mbio za polepole (Jogging), mashindano ya vyakula na ngoma za asili, maonesho ya shughuli za utamaduni na sanaa, mdahalo wa kukabiliana na mmomonyoko wa maadili pamoja maonesho ya filamu ya The Royal Tour katika kuunga mkono jitihada za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kuitangaza Tanzania.


Katika Tamasha hilo Mkoa wa Mwanza umeibuka Mshindi wa kwanza wa Ngoma za asili ukifuatiwa na Dodoma na namba tatu ni Mkoa wa Njombe, ambapo pia katika mashindano ya vyakula vya asili Mkoa wa Kilimanjaro umeibuka Mshindi ukifuatiwa na Iringa.


Katika hatua nyingine Tamasha la tatu la Utamaduni Kitaifa mwaka 2024, litafanyika katika Mkoa wa Morogoro mwezi Agosti ambapo Mkoa huo umesisitizwa kujiandaa vyema.

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.