• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MIAKA MITATU YA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UPATIKANAJI WA MAJI 91.6% WILAYANI MAKETE - DC SWEDA

Tarehe Iliyowekwa: March 26th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwajengea miradi ya Maji zaidi ya 17, wilayani humo, na kupelekea upatikanaji wa maji kwa asilimia 91.6.

Mhe. Sweda, amesema hayo leo, tarehe 25 Machi, 2024, wakati akiwa Mgeni rasmi katika kikao Cha wadau wa Maji Wilaya ya Makete, kilichofanyika ukumbi wa Bomani, ulipo katika Halmashauri hiyo.

"Miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imekuwa na tija sana kwa Wilaya ya Makete, ambapo kwasasa yanapatikana kwa asilima 91.6, tofauti na miaka ya nyuma na kupelekea wananchi kufurahia huduma hiyo" Alisema Mhe. Sweda.

Aidha Mhe. Sweda amewashukuru wananchi wa wilaya hiyo ya Makete, kwa kutunza vyanzo vya Maji sambamba na miradi mikubwa ambayo imejengwa kwenye maeneo yao.

Nae, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Njombe Ndg. Seleman Mdaba, amesema kuwa Mkoa huo umeweka mpango kazi ambao utawafanya wakazi wote Mkoa wa Njombe kufikiwa na maji safi na Salama kwa bei nafuu.

Kwa Upande wake, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Wilaya ya Makete, (RUWASA), Mhandisi Innocent Lyamuya amesema katika kufanikisha malengo yaliokusudiwa na serikali ya kutoa huduma ya Maji, wameunda vyombo vya utoaji huduma ya maji ngazi ya jamii ili kufanikisha ukusanyaji wa Ankara sambamba na utunzaji wa miradi hiyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Makete Mhe. Christopher Fungo, akihitimisha Kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Sweda, amewataka viongozi wa kata Wilayani humo, kushirikiana na watendaji wa mamlaka ndogo za maji, katika kata ili kutunza na kusimamia vyanzo vya sambamba na ukusanyaji wa Ankara za maji kwa ufasha kwa dhumuni la kuendeleza miradi ya maji iliyoletwa na Serikali.














ReplyForward


Add reaction










Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.