• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MKURUGENZI

Tarehe Iliyowekwa: April 23rd, 2022

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ndg. William Makufwe amewasimamisha kazi kwa muda watumishi wawili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili

Mkurugenzi huyo amechukua uamuzi huo hapo jana akiwa kwenye ziara ya Mikutano kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi Katika Kata ya Itundu, Matamba na Kinyika

Watumishi hao ni Mtendaji Kata ya Kinyika Lavenda Nyagoli ambaye anatuhumiwa na wananchi kwa kuwanyanyasa huku akiwatoza faini ambazo hazieleweki zimefanya jambo gani kwa mujibu wa Makubaliano ya Uongozi wa Kata na Wananchi

Wananchi wa Kata ya Kinyika wamemweleza Mkurugenzi Wilaya ya Makete kwamba wamekuwa wakinyanyaswa na Mtendaji huyo wa Kata pindi inapotokea changamoto na kuwaandikia faini kubwa kuliko uhalisia wa kosa lililofanyika na kufanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo kuwachapa viboko.

Pia Makufwe amemsimamisha kazi kwa Muda Mtendaji wa Kijiji cha Makusi Kata ya Itundu  Ndg. Musa Mwamgiga kwa kushindwa kuwasomea wananchi mapato na Matumizi kwa wakati huku ikielezwa kuwa ameshindwa kufanya kazi kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Kijiji Pamoja na Kamati ya Mipango na fedha ya Kijiji hicho

Viongozi wa Kamati ya Mipango na fedha ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndg. Yonamu Msigwa wamesema, Mtendaji wa Kijiji kila anaposhauriwa kuitisha vikao kujadili Mapato na Matumizi ya fedha za Kijiji amekuwa akiwakwepa wajumbe na kushindwa kukubaliana na Taarifa ya Mapato na Matumizi ya mwezi Julai, 2021 mpaka mwezi wa Desemba, 2021 aliyoisoma mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kwenye Mkutano na wananchi

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndg. Msigwa amesema “Kwa kweli Mkurugenzi tunakushukuru kwa kufika na kusikiliza kero zetu, kutokana na Mtendaji kukaa kwa zaidi ya miaka 13 hapa kijijini hakuna chochote alichofanya kwa ajili ya Maendeleo

Pia kila ninapomuagiza kuitisha Vikao ilia some mapato na Matumizi ananikwepa, sambamba na hii taarifa aliyoisoma hapa mimi sikubaliani nayo kama ambavyo wananchi wamekuwa na ukakasi wa Taarifa hii sambamba na Kamati ya fedha taarifa haijakaa saw ana kwa Pamoja tunaomba uondoke na Mtendaji huyu utuletee mwingine ili tuweze kufanya kazi za Maendeleo hapa Kijijini” Aliongeza Mwenyekiti wa Kijiji

 Baada ya kusikia malalamiko ya wananchi hao Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Afisa Utumishi Ndg. Avinus Kapinga na Mwanasheria wa Wilaya Ndg. Apollo Laizer wakakubaliana na maombi ya wananchi na kuagiza Mtendaji huyo kusimamishwa kazi kwa Muda mpaka uchunguzi utakapofanyika na Mkaguzi wa ndani

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Ndg. William Makufwe amesema “Namsimamisha kazi kwa muda Mtendaji huyu na Mkaguzi wa ndani atakuja hapa wiki mbili zijazo niwaombe wananchi mtoe ushirikiano na baada ya ukaguzi kukamilika tutatafuta Mtendaji mwingine”.

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.