• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MKURUGENZI MAKETE AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUTOKUWA CHANZO CHA MIGOGORO

Tarehe Iliyowekwa: January 18th, 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ndg. William M. Makufwe, leo Januari 18/2024, ameendelea ziara ya Ukaguzi wa uandikishaji wa wanafunzi kuanzia ngazi ya Awali, Msingi na Sekondari, pamoja na kusikiliza kero kupitia Kamati za Maendeleo ya Kata, katika kata mbili za Iniho na Luwumbu.

Akiwa katika ziara hiyo, Ndg. William M. Makufwe, amewataka viongozi wote kuanzia ngazi za vitongoji kushirikiana na watumishi wote wa serikali ambao wamepelekwa kwenye maeneo yao na si kuwa chanzo cha Migogoro, sambamba Usimamizi wa ukusanyaji wa Mapato ili serikali iendelee kuwapelekea miradi ya maendeleo.

Aidha, Ndg. Makufwe, amewaasa wasimamizi wa Taasisi za Elimu na Afya, kuilinda na kuisimamia vizuri miradi inayotekelezwa, na ambayo imekamilika ili iweze kuwa na faida kwa kizazi cha sasa na baadae, kwakuwa imetumia Fedha nyingi hadi kukamilika kwake.

Sambamba na hayo, Ndg. Makufwe, amewataka viongozi hao kuwa wa mfano katika kupambana na Udumavu kwenye maeneo yao, kwa kufuata maelekezo ambayo yamekuwa yakitolewa na Maafisa Lishe , ili Tanzania iwe na kizazi Bora cha sasa na baadae. 

Naye, Kaimu Afisa Lishe, wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Bi. Agnes Columbani, amewataka viongozi hao, kuhakikisha kuwa wanasimamia uanzishwaji wa Bustani za Mbogamboga pamoja na Ufugaji wa Kuku na wanyama wadogo wadogo kama vile Sungura, pamoja upandaji wa Miti ya Matunda, sambamba na kusimamia ulaji wa Mlo kamili kwa Watoto wadogo na wajawazito.

Kwa Upande wake, Diwani wa Kata ya Iniho, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mhe. Christopher Fungo, amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Kwa kufanya mikutano hiyo ambayo imekuwa na tija, pamoja na kuamua kushuka ngazi za chini kabisa ambazo viongozi wengi wameshindwa kufanya. 

Ikumbukwe kuwa, katika ziara hiyo, Ndg. Makufwe, aliongozana na Afisa Mapato, Ndg. Muyengi Bwire, Afisa Lishe, Bi. Agnes Columbani, ikiwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi kupitia KAMAKA, pamoja na wenyeviti wa Vitongoji, sambamba na kukagua Uandikishaji wa wanafunzi kuanzia ngazi ya awali.

Imeandaliwa na :

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

Halmashauri ya Wilaya ya Makete.














ReplyForward


Add reaction










Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.