• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

SERIKALI INATEKELEZA MIRADI MINGI NCHINI HUSUSANI WILAYANI MAKETE-DED MAKETE

Tarehe Iliyowekwa: April 7th, 2023

Ndg. William M. Makufwe Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Makete ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala Mikoa ya Tanzania bara (TOA) alisema Serikali imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali kwenye Serikali za Mitaa ikiwemo Wilaya ya Makete kwa lengo la kusaidia na kusogeza karibu huduma kwa Wananchi.

Makufwe alisema hayo akiwa kwenye mkutano wa mwaka wa TOA uliofanyika Dodoma tarehe 04-06/04/2023 ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mheshimiwa Angellah Kairuki.

Katika Mkutano huo Wakurugenzi walijadili namna ambavyo Serikali za mitaa zimefanikiwa kutekeleza majukumu vizuri katika shughuli mbalimbali za miradi ya Maendeleo ikiwemo katika Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe kwa kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi kupitia miradi mbalimbali ya Maendeleo na Wananchi kuona manufaa ya miradi hiyo.

Katika Hotuba yake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mheshimiwa Angellah Kairuki amesema, Serikali imendaa Sera ya Ugatuaji wa Madaraka (D by D) ambayo iko katika hatua ya mwisho ya mapitio inayotarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Mheshimiwa Kairuki ameyasema hayo Aprili 4, 2023 jijini Dodoma wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika Mkutano Mkuu wa 13 wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA).

"Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuhusu Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG), ulikuwa ni mfumo muhimu kwa ajili ya kupeleka fedha za maendeleo kwenye Mamlaka za Serikali Mitaa (MSM) Tanzania Bara, kama nyenzo ya utekelezaji wa ugatuaji wa madaraka sehemu ya fedha,"amefafanua Waziri Kairuki.

Pia amesema,tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004/2005, mfumo huo ulichangia kwa kiasi kikubwa kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Aidha,ulileta msukumo kwenye maeneo ya utendaji wa Majukumu ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo mipango, bajeti, usimamizi wa fedha pamoja na sekta nyingine kama Afya, Elimu, Maji na Kilimo.

"Mfumo wa LGDG ulikuwa mfano wa kuigwa kwa ufadhili wa uwekezaji wa ndani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, kulikuwa na ongezeko la upatikanaji wa rasilimali fedha za maendeleo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na ndiyo ruzuku iliyowezesha kukamilisha maboma yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.

"Ndiyo ruzuku iliyotumika kuendesha ofisi na kujenga uwezo wa watendaji katika ngazi za kata,vijiji na mitaa na ndiyo fedha zilizotumika katika ufuatiliaji wa miradi kwa uhakika na kutekeleza miradi iliyoibuliwa na jamii,"amebainisha Waziri Kairuki.

Mheshimiwa Waziri Kairuki amesema, Mfumo wa LGDG ulihuishwa mwaka 2015/2016 na ulipaswa kuanza mwaka 2016/2017.

Hata hivyo, amesema Serikali ilikuja na mpango wa miradi ya kimkakati kwa lengo la kuzalisha mapato katika Halmashauri ili ziweze kujiendesha na kusitishwa kwa mfumo wa Ruzuku ya Maendeleo katika Serikali za Mitaa.


Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.