• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MKUU WA WILAYA

Tarehe Iliyowekwa: May 12th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh. Juma Sweda akiwa kwenye mkutano uliojumuisha viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali amewasihi  kuendelea kuhamasisha waumini kutambua juu ya umuhimu wa zoezi la Sensa pamoja na Anuani za makazi.

Mh. Sweda alitoa rai hiyo kwa Viongozi wa Jukwaa la kikristo Makete walipokutana katika Kanisa Katoliki Makete Mjini kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali yanayohusu madhehebu yao ikiwemo kuendelea kusisitiza uwepo wa amani na upendo nchini.

Mkutano huo ulijadili maendeleo ya Jukwaa la kikristo Wilayani Makete sambamba na kuzungumzia zoezi la anuani za makazi pamoja na kuhimiza wananchi kuweka Vibao kwenye nyumba zao.

Mkuu wa Wilaya alisema kwa sasa Serikali imetunga sheria pamoja na adhabu kwa wale ambao hawatazingatia uwekaji wa vibao vya anuani za makazi, hivyo kushindwa kufanya hivyo kwa muda uliopangwa atatakiwa kulipa faini isiyozidi shilingi laki tatu (300,000) au kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela au vyote kwa pamoja.

“Niwaombe wachungaji, Mapadre na viongozi wa dini zote tunapokutana na waumini wetu huko kwenye madhehebu wakati wa ibada na hata nje ya ibada tuwaelimishe kuhusu umuhimu wa Anuani za Makazi na zoezi la Sensa ambalo litafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima”.

Mwenyekiti wa jukwaa la kikristo wilaya ya Makete Padre Laurian Kayombo alibainisha baadhi ya changamoto ambazo wananchi wamekuwa wakikumbana nazo ili Serikali iweze kuwasidia kuondokana na changamoto hizo ambazo waumini wetu wanakutana nazo ikiwemo kukatika umeme mara kwa mara bila taarifa na kuwasababishia hasara ya kuungua vifaa vyao, Barabara nyingi kutopitika kipindi cha mvua na wananchi kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo kupeleka mazao sokoni”.

“Tunakushukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuzungumza na viongozi wa Dini, kuhusu zoezi la Anuani za makazi pamoja na Sensa kwani Serikali imekuwa ikituelekeza na tunayafanyia kazi maelekezo hayo tunaamini waumini watazidi kupata elimu kupitia ibada tunazofanya” ameongeza Padre Kayombo.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Viongozi wengine Mkuu wa Jimbo la Iwawa KKKT-DKK Mchungaji Mathayo Sanga, amesema wapo tayari kushirikiana na Mkuu wa Wilaya katika kuhimiza zoezi la Anuani za Makazi na Sensa pamoja na kuendelea kuihubiri amani ya nchi katika nyumba za ibada.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA April 25, 2022
  • TANGAZO LA KAZI ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 May 06, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA KAMATI YA SENSA

    May 24, 2022
  • KIKAO CHA KAMATI YA SENSA

    May 24, 2022
  • KIKAO CHA KAMATI YA SENSA

    May 24, 2022
  • KIKAO CHA KAMATI YA SENSA

    May 24, 2022
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • MAKETE DC Online TV
  • MAKETE DC Instagram page
  • PLANREP
  • MAKETE DC Facebook page
  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • BEMIS
  • HIMS
  • FFARS

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.