• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

SAMAKI ADIMU DUNIANI WANAOPATIKANA MAKETE

Tarehe Iliyowekwa: September 13th, 2022

Samaki adimu Duniani wanaopatikana Wilayani Makete katika mito mbalimbali inayozunguka Wilaya ya Makete wanaofahamika kwa jina la Solomoni (Salmon)

Peter Soyala kutoka Idara ya Maliasili na Mazingira Wilaya ya Makete anatufahamisha maajabu ya kuhusu Samaki huyu adimu Duniani

Huyu ni samaki aliye maarufu sana diniani, Ukiachana mbali na kuwa na minofu pia mafuta ya samaki huyu ni mujarabu katika kulinda afya ya mwili dhidi ya maradhi pamoja na kusaidia ukuaji mzuri wa mwili na akili hususan kwa watoto wadogo.

Samaki huyu anapatikana sana kwenye mito iliyopo Amerca ya Kaskazini (North Amerca) na wakoloni waliopandikiza pia katika mito mbalimbali ya Wilaya ya Makete nchini Tanzania, samaki hawa maarufu wanapatikana kwa wingi sana katika mto Luvanyina kwa Makete na mito mingine mikubwa.

Miongoni mwa maajabu ya samaki hawa ni safari yao ndefu ya kutembea kutoka mtoni kwenda baharini au Ziwani na kurejea tena walipo toka baada ya kukaa muda mrefu wakiwa baharini au ziwani.

Samaki huyu anasifa ya kuishi kwenye maji baridi na maji ya chumvi. Maisha ya samaki hawa yanaanzia pale samaki jike anapotaga mayai maeneo ya juu ya mto amapo kuna maji yabaridi (yasiyo na chumvi). Baada ya kutotolewa kwa samaki hawa wanakaa mtoni hapa kwa muda kadhaa.baada ya kwisha kuuwa kiasi cha kuweza kujitafutia chakula wenyewe na kuweza kujilinda hapa wanaanza safari yao ya maajabu sana.

Salmon baada ya kukuwa na kukomaa anaanza kusogea karibu na bahari au Ziwa, na hapa mabadiliko huanza kutokea kwenye mwili wake ili kuweza kumfanya aishi kwenye maji ya chumvi.

Baada ya kuweza kuendana na mazingira ya maji ya chumvi na hali ya hewa salmon wanaanza safari yao ya kuelekea baharini ambapo watakaa kwa muda mrefu sana.

Safari ya samaki hawa inaweza kuwa na urefu kuanzia kilomita 1600 mpaka kilomita 4000 inategemea aina ya samaki hawa. Inakadiriwa kuwa wakati wa safari yao samaki hawa huweza kutembea kwa umbali wa kilomita 6 mpaka 7 kwa siku.

 Baada ya kizazi hiki kuhamia baharini na kukaa kwa muda wa miaka kadhaa, samaki hawa wanapotaka kutaga na ili kuendeleza kizazi wanarudi kule walipozaliwa yaani mtoni. Na hapa safari ya kurudi iliyo na maajabu ndipo huanzia.

Itambulike kuwa samaki hawa wanatakiwa kurudi pale walipozaliwa na haijalishi ni muda gani toka waondoke lakini lazima watafika. Pia kwa kuwa maji ya mto yanaelekea baharini na samaki hawa wanarudi mtoni walipozaliwa basi safari yao itakuwa inapingana na maji ya mtu. Hivyo itawalazimu kukinzana na nguvu ya maji ya mtu na wakati mwingine wanapokutana kwenye maporimoko ya maji wanatakiwa waruke.

Safari hii imejawa uvumilivu kwani kuna wanyama walao samaki huwa wanawasubiria maeneo haya yenye maporomoko pindi wanaporuka wawale. Samaki hawa wanaweza kuruka maporomoko yenye urefu unaokadiriwa kufikia mita 3. Pia Salmon anaweza kukutana na sehemu ya mto ambayo ina maji kidogo aya pamekauka, samaki huyu anaamuwa kuruka ili ayapate maji ama atasubiria mpaka maji yaingie aendelee na safari yake.

Wataalamu wanatueleza kuwa mnyama huyu aaweza kupajuwa mtoni alipo zaliwa kwa kutumia harufu ya maji. Inaelezwa kuwa samaki hawa wanaweza kutofautisha harufu za maji hata kwa kiwango kidogo sana. Samaki huyu pindi anapozaliwa kule mtoni harufu na maji ya eeo alipozaliwa anakuwa na kumbukumbu nayo bila ya kujali amekaa baharini kwa muda gani.

Salmon baada ya safari ndefu na iliyo ngumu anarudi mtoni ambapo amezaliwa. Salmon akiwa kwenye safari yake mwili wake hufanya babadiliko ambauo yatamfanya aweze kuishi kwenye maji ya baridi. Hii ni tofauti na samaki wengine ambao ukimtoa maji ya baridi papo kwa papo na ukamtia maji ya chumvi hufa. Salmon ana uwezo wa kuishi mazingira yote haya.

Baada ya kuwasili mtoni pale walipozaliwa samaki hawa wanataga mayai na kuyatotowa. Makinda yanapototolewa yanakuwa hayana uwezo wa kujilinda hivyo wanajificha kwenye mawe, baada ya wiki kupita hatimaye samaki hawa wanaweza kujitaftia chakula wenyewe safari hii huanza tena. Na haya ndio maisha ya samaki huyu salmon.

Nani kamfundisha samaki huyu kuweza kujuwa mazingira na maeneo alozaliwa, na kuweza kurudi bila ya kukosea. Kwa nini samaki huyu anatembea safari hii iliyo na ugumu na uvumilivu?. Salmon ni samaki ambaye anatupatia mafunzo mengi sana. Kwa mfano sikuzote kabiliana na changamoto kwani kukimbia zio njia sahihi ya kutatua tatua tatizo. Salmon anaenelea na safari yake bila ya kujali nguvu ya maji ya mto kuwa itamrudisha baharini, au maadua walao samaki ama maporomoko ambayo hataweza kuyaruka.

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA AWATAKA WASIMAMIZI WA MIRADI YENYE FEDHA KUKAMILIKA KWA WAKATI

    June 05, 2025
  • DED MWAGA AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI KWENYE MIRADI KIKAMILIFU

    June 04, 2025
  • MAKETE IPO TAYARI KWA BBT

    May 26, 2025
  • WENYEVITI WA VIJIJI NA VITONGOJI WILAYANI MAKETE WATAKIWA KUFUATA ASHERIA, KANUNI NA MAADILI YA KAZI

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.