• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

TAASISI ZA SERIKALI NJOONI NA MAWAZO MBADALA KUUINUA UCHUMI WA MAKETE- MHE SWEDA

Tarehe Iliyowekwa: December 1st, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Juma Sweda, amewataka watalaam kutoka taasisi mbalimbali za serikali zilizopo, Halmashauri ya wilaya ya Makete, kuhakikisha kuwa wanakuja na mkakati mpya wa kupata mapato ya kutosha bila kutegemea maeneo ya kilimo na wafanyabiashara.

Mhe. Juma Sweda, amesema hayo leo, Desemba 1, 2023, wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri (DCC), kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Bomani, kuwa wilaya ya Makate ni tajiri, inahitaji kutafutwa wawekezaji ili halmashauri iweze kupata mapato ya kutosha.

Sambamba na hayo, Mhe. Sweda amewataka TARURA kutatua changamoto za miundombinu ya barabara, kutoka Ikuwo kuelekea Matamba ili kuwasaidia wakazi wa Ikuwo, ambao wamekuwa katika sintofahamu ya usafiri kwa muda mrefu.

Pia, Mhe.Sweda amewataka wakazi wa Wilaya ya Makete, kuhakikisha kuwa wanapambana ongezeko la Utapiamlo wilayani humo, ikiwa ni kampeni endelevu ya kumkomboa mtoto na ongezeko la Udumavu hapa nchini.

Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mhe. Christopher Fungo, ameshukuru kufanyika kwa kikao, na kwamba wameyachukua wataenda kuyafanyia kazi ili wananchi waweze kuhudumiwa vizuri.

Akijibu baadhi ya hoja za wadau katika kikao hicho, DCC, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. William M. Makufwe, amewataka wafanyabishara wa Makete kusajiliwa kwenye mfumo wa TAUSI, ikiwa ni pamoja na kupewa elimu ya umuhimu wa kulipa kodi pamoja na mapato ya halmashauri.

Aidha, Ndg. Makufwe, amesema kuwa wameshaomba maghala manne ambayo yatatumika katika kuhifadhia Ngao, kutokana na kuwepo kwa ongezeko la mavuno ya zao hilo, ambalo limeonekana kuwa mkombozi kwa wakulima wilayani Makete, ikiwa ni pamoja na kutaka kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kusindika zao hilo.

Wakichangia kwa nafasi tofauti, baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo, akiwepo Afisa Manunuzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. Mathias Mbafu, amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuwezeshwa mikopo, ambayo itawasaidia kununua mashinde ndogo ndogo, ambazo zitawasaidia kuchakata mazao mbalimbali kama vile ngano.

Hata hivyo, kikao cha Kamati ya Ushauri wilaya ya Makete, DCC, kimehitimishwa kwa kuundwa kwa kamati ya ambayo itachakata fursa mbalimbali za uwekezaji, wilayani humo ili wilaya hiyo iweze kufunguka kiuchumi.

Imeandaliwa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Halmashauri ya Wilaya ya Makete.

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.