• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

TARI YARIDHIA KUJENGA KITUO CHA UTAFITI WA MBEGU MBORA ZA KILIMO CHA VIAZI MVIRINGO NA TUFAA WILAYANI MAKETE

Tarehe Iliyowekwa: September 10th, 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo hapa nchini (TARI), Dkt, Thomas Bwana, leo Septemba 10,2025, akiwa ameongozana na Wataalam mbalimbali kutoka katika taasisi hiyo wamekagua maeneo katika Kijiji cha Ibaga pamoja na Iniho, na kuridhia kuanzisha kituo cha Utafiti wa mbegu za viazi Mviringo pamoja na Tufaa. 

Akizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya ukaguzi wa maeneo hayo, Dkt, Bwana, amesema kuwa hakuna haja ya kuendelea kuchelewa kuanzishwa kwa kituo hicho cha Utafiti wa Mbegu za Kilimo bora, kutokana na umuhimu wake pamoja na uhitaji wa mbegu hizo za wakulima.

“hakuna haja ya kumcheleweshea mafanikio mkulima,mkulima hatakiwi kuwa nasababu ya kujitetea kuwa amekosa mbegu bora za kilimo, au wataalam wa kilimo, hata kama akipata changamoto za uzalishaji tunatakiwa kuwepo ili kuwasaidia kwakuwa ndio jukumu letu”   alisema Dkt. Bwana.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg, Jerry Daimon Mwaga, amesema kuwa lengo la halmashauri ni kuhakikisha kuwa wanatafuta fursa mbalimbali za masoko pamoja na kuboresha kilimo kwa wakulima ili waweze kukua kiuchumi.

“Halmashauri imedhamiria kuhakikisha kuwa inaboresha mazingira ya uzalishaji wa mazao ndani ya wilaya ya Makete, ndio maana imekuwa ikitafuta fursa mbalimbali za uboreshaji wa kilimo  kutokana na mchango wao mkubwa katika uchumi wa Makete, hivyo tunaaamini TARI mtachangia kwa sehemu kubwa katika utafiti wa Mbegu bora za viazi Mviringo pamoja na Tufaa” alisema Ndg, Mwaga.

Naye Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ndg. Evance Mdee, amesema kuwa zaidi ya ekari 600 zimetengwa kwa ajili ya Uwekezaji wa Utafiti wa  Mbegu bora za Kilimo cha viazi mviringo katika vijiji vya Malembuli na Ibaga, ikiwa ni pamoja na mpango wa uwekaji wa mifumo ya umwagiliaji ili wakulima hao waweze kulima katika misimu yote ya kilimo.

Ikumbukwe kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Makete, asilimia 90 ya wakazi wake ni wakulima, na kilimo kimekuwa kikichangia kwa sehemu kubwa katika kukuza uchumi wa wananchi, hivyo Halmashauri imepanga kuhakikisha kuwa wakulima wanajengewa mazingira bora ya uzalishaji wa mazao yao pamoja na masoko.

 

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 September 01, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MAKETE DC AAGIZA KUKAMILIKA HARAKA KWA NYUMBA PACHA YA WATUMISHI KITUO CHA AFYA KIPAGALO

    September 11, 2025
  • TARI YARIDHIA KUJENGA KITUO CHA UTAFITI WA MBEGU MBORA ZA KILIMO CHA VIAZI MVIRINGO NA TUFAA WILAYANI MAKETE

    September 10, 2025
  • DED MAKETE AWATAKA WATUMISHI WAPYA KUYAISHI MAADILI YA KIUTUMISHI WA UMMA

    September 02, 2025
  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.