• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

TUENDELEE KUWALEA VIJANA KATIKA MAADILI

Tarehe Iliyowekwa: October 1st, 2022

Wazee Wilayani Makete wamekumbushwa kuendelea kuwalea vijana katika Misingi ya maadili ili kuwa na Taifa la Vijana wachapa kazi na waliostaarabika.

Hayo yamesemwa leo 1 Octoba, 2022 na Mtendaji Kata ya Ukwama Absalom Mwenga katika maadhimisho ya wazee Duniani yaliyofanyika katika Kijiji cha Ukwama Kata ya Ukwama Wilayani Makete Mkoani Njombe.

Mwenga amesema wazee wanao wajibu wa kuhakikisha vijana wanakuwa katika maadili mema na misingi ya kujiletea maendeleo katika shughuli zao za kila siku ili waweze kuwasaidia wazee wao katika kuwapatia mahitaji muhimu ya kibinadamu.

Mwenga ameongeza kuwa wazee wanaumuhimu mkubwa kwenye Jamii katika kuelimisha vijana kuhusu Maadili, Elimu, Afya na mambo mbalimbali katika jamii wanayoiishi.

Afisa Maendeleo Kata ya Ukwama Columba Mgeyekwa akiwa katika Maadhimisho hayo amesema kulingana na hali ya uwepo wa Ugonjwa wa UVIKO-19 Duniani wazee wanasisitizwa kupata chanjo ya UVIKO-19 ili kujikinga na ugonjwa huo hatari

Amewasihi wazee kwamba ili kuwa na Taifa imara inahitajika kuwa na watu wenye Afya njema ikiwemo wazee waliopata chanjo ya UVIKO-19

Kuhusu kuwalea vijana katika maadili wazee wa Kijiji cha Ukwama wamesema "tuendelee kuwalea vijana wetu katika maadili kwa kuwa vijana wengi wanazidi kupoteza uhalisia wa Utanzania na kuenea kwa mmonyoko wa maadili ya mila zetu".

Pia wasemwasihi vijana kutenga muda wa kuzungumza na wazee ili kupata ujuzi wa namna ya kuendesha shughuli zao kihalali bila kuwa na matukio mabaya katika jamii na kuchota busara za wazee.

Wakati huohuo wazee hao wameiomba Serikali kuendelea kuwaandalia Kadi za Afya ili ziweze kuwasaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa urahisi wanapokuwa wamepatwa changamoto za kiafya.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wazee mwaka huu ni Ustahimili na umahiri wa wazee ni Msingi wa Maendeleo ya Taifa

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.