• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WAKAZI WILAYANI MAKETE WATAKIWA KUUENZI MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR KIVITENDO

Tarehe Iliyowekwa: April 24th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Juma S. Sweda, amewataka wakazi wa Wilaya hiyo, kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutokana na umuhimu wake kiuchumi, kiutamaduni na uwepo wa amani baina yao.

Mhe. Sweda, amesema hayo leo, Aprili 24, 2024, mara baada ya kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Makete, ikiwa ni njia mojawapo ya kuadhimisha miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Muungano huu ni tunu ambayo tumeachiwa na viongozi wetu, ambao ni waasisi wa taifa hili, Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume, ambao walifanya haya ikiwa njia mojawapo ua kukuza uchumi, umoja na amani baina ya Tanzania bara na Visiwani” alisema Mhe. Sweda.

Aidha, Mhe. Sweda, amewashukuru watumishi pamoja na wananchi ambao wamejitokeza kwa wingi kufanya usafi katika Hospitali hiyo ya Wilaya ya Makete, sambamba na kufanya matendo ya huruma kwa wagonjwa ambao wamelazwa hospitalini hapo.

Kwa Upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. Humphrey Mushi, amesema kuwa wameamua kufanya matendo ya huruma kama madhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika Hospitali hiyo ya Wilaya ya Makete.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora, kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Irene Chilewa, amesema kuwa miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, umekuwa na tija katika kada hiyo kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi pamoja na ujenzi wa vituo vya Afya na Hospitali za kutosha hapa nchini.

Ikumbukwe kuwa miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mwaka huu kitaifa itafanyika katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo kwa wilaya ya Makete maadhimisho hayo yameanza kufanyika kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama vile usafi katika Hospitali ya Wilaya pamoja na upandaji miti kwenye ameneo ya wazi, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema kuwa “Tumeshikamana na Tumeimarika, kwa Maendeleo ya Taifa letu”.

Imeandaliwa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Halmashauri ya Wilaya ya Makete.

 

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.