• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WANANCHI MAKETE WATAKIWA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI KWA KUPANDA MITI RAFIKI

Tarehe Iliyowekwa: February 14th, 2024

Wananchi Wilayani Makete mkoani Njombe, wametakiwa kutunza vyanzo vya maji katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutofanya shughuli mbalimbali za kibinadamu katika maeneo hayo kama vile kilimo pamoja na kukata miti hovyo, sambamba na kupanda miti isiyo rafiki na maji.

Wito huo umetolewa na Ndg. Nyairobi Sayi Masalu kutoka Ofisi ya Mazingira , Halmashauri ya Wilaya ya Makete, wakati wa zoezi la upandaji wa miti aina ya Mzambarau kwenye chanzo cha maji eneo la Dombwela B lililopo Kata ya Iwawa, Wilayani Makete. 

"Acheni kupeleka wanyama kwenye vyanzo vya Maji, hususani Ng'ombe na mifugo mingine kwakuwa mnaharibu vyanzo hivyo, na kupelekea kukosa Maji Kwa siku za mbeleni" Alisema Ndg. Masalu.

Aidha, Ndg. Masalu amesema kuwa, wao kama ofisi ya mazingira watawachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaoendelea na shughuli za ufugaji na Kilimo kwenye vyanzo vya maji kwakuwa sheria inairuhusu kuanzia mita 60 kutoka chanzo cha Maji.

Naye, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Iwawa ambae pia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Dombwela Mhe. Joseph Mbilinyi ameishukuru ofisi ya mazingira Makete kwa utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira na amewataka wananchi kuacha mara moja kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji kwani kumekuwa na uharibifu mkubwa unaotokana na kazi hizo. 

Nao baadhi ya wananchi, wakiwemo wafugaji waliofika katika zoezi hilo la upandaji wa miti kwenye chanzo hicho akiwemo Bw. Boniface Kyando, amesema kuwa upandaji wa miti katika eneo hilo utasaidia kwa kiasi kikubwa utunzaji wa chazo hicho, ambapo ametoa wito kwa wananchi kutopekleka mifugo yao katika eneo hilo kutokana na uharibifu unaowezajitokeza katika chanzo hicho.

Ikumbukwe kuwa, miti zaidi ya sabini imepandwa katika eneo hilo huku ofisi ya mazingira Wilayani Makete, ikisema kuwa zoezi hilo la upandaji wa miti katika vyanzo vya vya maji hapa Wilayani Makete ilitakuwa endelevu, na kwamba maeneo mengine pia yatafikiwa hivi karibuni.

Imeandaliwa na:

Kitengo cha Mawasiliano, 

Halmashauri ya Wilaya ya Makete.












Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.