• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WANUFAIKA WA MIKOPO WATAKIWA KUZITUMIA FEDHA HIZO KWENYE MIRADI ILIYOKUSUDIWA

Tarehe Iliyowekwa: December 31st, 2024

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mhe. Christopher Yonam Fungo, leo Desemaba 31, 2024, amewataka wanufaika wa mikopo ya asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri, kuhakikisha kuwa wanatumia fedha hizo kwenye malengo yaliyokusudiwa na vikundi vyao ili ziwe na tija kiuchumi.  

Mhe. Fungo, amesema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Utoaji wa mikopo hiyo, kiasi cha shilingi milioni 449,000,000.00, ambayo imefanyika katika ukumbi wa Bomani, uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Makete.

“Fedha hizi mnazopewa leo sio hisani, nendeni mkazifanyie kazi iliyokusudiwa ili ziwe na tija katika maisha yenu, sitegemei kuona baadae tunaanza kutafutana kwamba kuna vikundi vimeshindwa kurejesha, haifurahishi, kwahiyo hakikisheni mnazitumia vizuri kama malengo ya kikundi yanavyotaka” alisema Mhe. Fungo.

Aidha, Mhe. Christopher Yonam Fungo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuweka mfumo mzuri wa utolewaji wa mikopo hiyo, ambayo hapo awali ilionekana kuwa na changamoto katika urejeshaji wake.

Kwa Upande Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. William M. Makufwe, amesema kuwa, vikundi vimekuwa vikitumia fedha tofauti na kusudio na kupelekea changamoto katika urejeshaji, sambamba na kutokakaa vikao ambavyo vingeweza kuwasaidia kutatua changamoto ambazo wanakutana nazo katika utekelezaji wa mipango yao.

Pia,   Ndg. Makufwe, ameabainisha kuwa, Halmashauri imetoa kiasi cha shilingi milioni 449, ikiwa ni awamu ya kwanza ya utolewaji wa mikopo hiyo, kwa vikundi 52, ambayvo vinatoka katika kata 10, na kwamba awamu ya pili itatolewa zaidi ya milioni 500, kwa vikundi ambavyo vitakuwa viemekidhi matakwa ya utolewaji wa mikopo hiyo.

Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM, Wilaya ya Makete, Ndg. Tamson Mbilinyi, ameseama kuwa, utolewaji wa mikopo hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na uwezo wa kujiendeleza kiuchumi.

Ikumbukwe, kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 449, kwa vikundi 52 kutoka kwenye kata 10, ambapo vikundi vya Vijana vipo 24, Wanawake vikundi 26, na Watu wenye Ulemavu vikundi 2, ikiwa ni awamu ya kwanza ya utolewaji wa mikopo hiyo.

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA - UTOLEWAJI WA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI 2025-2026 November 16, 2025
  • MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 September 01, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA AAGIZA KUKAMILISHA MIRADI KWA HARAKA

    November 26, 2025
  • MKURUGENZI MTENDAJI MAKETE DC , JERRY MWAGA, AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII

    November 13, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MAKETE MHE. KISSA KASONGWA AWATAKA WAFANYABISHARA WILAYANI HUMO KUWEKEZA NYUMBANI

    November 12, 2025
  • DED MWAGA AONGOZANA NA MENEJA TARURA KUKAGUA BARABARA YA MANG'OTO IBAGA

    November 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.