• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WATUHUMIWA KUHUJUMU MBOLEA YA RUZUKU MAKETE

Tarehe Iliyowekwa: September 21st, 2022

Picha wa kwanza kutoka kulia ni Afisa Udhibiti ubora wa Mbolea kutoka Kanda Nyanda za Juu kusini Henerico Renatus Kiagala, akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete William M. Makufwe,  Mwanasheria kutoka wakala wa Mbolea nchini (TFRA) Godfrey Munisi na wa mwisho kushoto ni mtaalamu kutoka Idara ya Kilimo Makete Lazaro Kasebwa baada ya kufanya ufatiliaji kuhusu mwenendo wa zoezi la uuzaji wa mbolea ya Ruzuku Wilaya ya Makete.

Wakulima wawili wilayani Makete wamekamatwa kwa tuhuma za ubadhirifu na kuhusishwa kuhujumu zoezi la Mbolea za Ruzuku.

Hii ni kufuatia kuwepo Mkanganyiko wa taarifa za ununuzi wa mbolea uliobainika kupitia mfumo wa ununuzi wa mbolea unaofanywa na Serikali.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete William M. Makufwe akiwa na Katibu Tawala Wilaya ya Makete Grace Mgeni, Afisa Kilimo Wilaya ya Makete, Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Makete, Afisa Udhibiti ubora wa Mbolea kutoka Kanda Nyanda za Juu kusini Henerico Kiagala, Mwanasheria kutoka wakala wa Mbolea nchini (TFRA) Godfrey Munisi, amesema mbolea inayouzwa kwa Ruzuku imeonekana kuwa na changamoto ya uaminifu kwa baadhi ya wakulima na wasambazaji wa Mbolea na wameamua kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa zoezi hilo.

Watuhumiwa katika tuhuma hizo ni Husein Ashery Mwalyoyo alisajiliwa kwenye mfumo Kata ya Matamba_Wilayani Makete kama mnufaika kwa ekari 30 ambapo angestahili kupata mbolea ya ruzuku mifuko 60 ya kilo 50

Katika mfumo ambao ndio utatumika kuwalipa mawakala inaonesha kuwa amenufaika mifuko 240 ya mbolea badala ya mifuko 60

Baada ya kumhoji amesema yeye amepata mifuko 120 toka kampuni ya Premium ya Makambako.

Mkurugenzi amesema, kwa eneo la Matamba yupo wakala aliyepewa kazi hiyo ya kusambaza na kuuza Mbolea ya Ruzuku, kitendo cha kwenda Makambako ni kiashiria tosha kuwa alikuwa na nia ovu.

Pia mkulima Frolida Edson Sanga wa Kinyika ambapo ni Kijiji jirani na Matamba alisajiliwa kunufaika ekari 25 sawa na mifuko 50 ya mbolea, ambapo kwenye mfumo inaonesha amenufaika mifuko 140, ambapo ni sawa na mifuko 90 zaidi ya alichostahili kupewa.

Baada ya kumhoji amesema amepewa mifuko 105 na wakala Premium wa Makambako wakati mkulima ni wa Makete.

Inaonesha wazi kuna hujuma zimefanyika kwa hawa wakulima wakishirikiana na huyo wakala.

"Wasiwasi unaonyesha kuhujumu kutokana na mkanganyiko wa taarifa ambapo wakala baada ya kuhojiwa anasema alimpa mkulima Mifuko 200, lakini Mkulima anasema amepata mifuko 120 wakati kwenye mfumo inaonyesha  mkulima amenunua mifuko ya mbolea 240...kwa hiyo hii inatia mashaka" William Makufwe Mkueugenzi Mtendaji Makete

Kwa upande wake Afisa Udhibiti ubora wa Mbolea kutoka Kanda Nyanda za Juu kusini Henerico Renatus Kiagala amesema mpaka sasa watuhumiwa wawili wamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu mashataka yanayowakabili.

KUTAZAMA VIDEO BONYEZA HAPA

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.