• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII, MHE,DKT.PINDI CHANA, AAGIZA KUUNDWA VIKOSI KAZI KWENYE VIJIJI, KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO

Tarehe Iliyowekwa: October 8th, 2024

Waziri wa Mali Asili na Utalii nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Pindi Chana, ameagiza kupatikana kwa majina ya vijana katika kila kijiji Wilayani Makete, ambako kumekuwa na uharibifu mkubwa wa uchomaji moto hovyo, ambao watapewa mafunzo ya Ulinzi wa Mali Asili na Utunzaji wa Mazingira.

Mhe. Dkt. Pindi Chana, amesema hayo leo, Oktoba 8,2024, wakati ametembelea makao makuu ya Wilaya ya Makete, na kukutana na Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Juma S. Sweda, pamoja Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. Humphrey Mushi.

“Maagizo ya Mheshimiwa Rais ni kuwa kila kijiji kiwe na Game Scout Village, (GSV), ambao watakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa kunakuwa na usalama wa Mali Asili zetu zilizopo vijijini ili kupunguza changamoto hizi za uchomaji miti hovyo” Alisema Dkt. Pindi Chana.

Aidha, Waziri Chana, ameagiza kukaguliwa kwa Sheria ndogo zilizoundwa, kama zinakidhi ili ziweze kutumika katika kuwachukulia hatua wale wote ambao wamekuwa wakiharibu mazingira sambamba na kutia hasara kwa wamiliki wa miti.

Kwa upande Mwingine, Waziri huyo wa Mali Asili na Utalii, ameagiza Idara za Kilimo, Mali Asili na Mazingira kuhakikisha kuwa wanatoa elimu ya kutosha kuhusu namna bora ya Uandaaji wa Mashamba pamoja na madhara ya uchomaji miti hovyo, na kwamba agenda ya uchomaji moto iwe ya kila kikao.

Pia Waziri Pindi Chana, ameagiza Mamlaka za Utafiti wa Misitu, kama vile TAFORI, kuhakikisha kuwa wanafanya tafiti ambazo zitapunguza matumizi makubwa ya ukataji miti ya asili kwa ajili ya mkaa, kwa kubaini miti ya kupanda ambayo itakuwa inatumika katika uchomaji mkaa.

Kwa Upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Juma S. Sweda, amemshukuru waziri huyo, na kwamba wamepokea maagizo na watayafanyia kazi kama wilaya, ili kuhakikisha kuwa uharibifu wa mazingira kupitia uchomaji moto hovyo haujirudii tena.

Hata hivyo, Afisa Mali Asili na Mazingira, Wilaya ya Makete, Ndg. George Gujonjo, akisoma taarifa ya uchomaji moto hovyo, mbele ya Waziri wa Mali Asili na Utalii, Mhe. Dkt. Pindi Chana, amesema kuwa, zaidi ya ekari 1960, zenye thamani ya Tsh. 1,494,653,942, zimechomwa moto, na kupelekea hasara kubwa kwa wamiliki wa misitu ya Kupanda na Asili.

 Imeandaliwa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, 

Halmashauri ya Wilaya ya Makete 

 

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.