• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za Watumishi |
Makete District Council
Makete District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, takwimu na ufuatiliaji
      • Ujenzi
      • Usafi na mazingira
      • Finance and Trade
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wazee na watoto
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Agriculture, irrigation and Coorparation
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya habari na mawasiliano
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo na nyuki
    • Utalii
    • Viwanda
    • Nishati ya umeme
    • Maliasili
    • Usambazaji maji
    • Elimu
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • madiwani
    • orodha ya madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance, Planing and Administration
      • Elimu, afya na maji
      • Economic, Works and Envornment
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya vikao vya halmashauri
      • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
      • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuonana na wananchi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
      • Kauli ya Serikali kuhusu 1.5 Trioni
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MHE. DKT. SELEMEMAN SAID JAFO, ASISITIZA AMANI, UPENDO NA USHIRIKIANO KATIKA UKUZAZI WA UCHUMI NCHINI

Tarehe Iliyowekwa: February 19th, 2025

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Seleman Said Jafo, leo Februari 19,2025, ametoa rai kwa wakazi wa mkoa wa Njombe, kuendeleza na kusimamia ipasavyo utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati iliyopo mkoani humo ili iweze kuwa na tija kwa taifa na watanzania kwa ujumla.

Mhe. Dkt. Jafo ametoa rai hiyo, wakati akiongea kwenye Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Mkoa wa Njombe, ambao umefanyika kwenye Ukumbi wa mikutano uliopo kwenye  Ofisi za Mkuu wa Mkoa huo zilizopo Mtaa wa Lunyanyi, mjini Njombe.

“Kuna Nchi hapa Duniani hawaamini kama Tanzania inawewa kuwa na miradi mkakati Mikubwa ya maendeleo yenye uwezo wa kuliletea taifa faida kiuchumi, hivyo nendeni mkawekeze ikiwa ni pamoja kusimamia vizuri miradi iliyopo, na ile ambayo inatekelezwa ikatimie kwa faida ya Taifa letu” alisema Dkt. Jafo.

Aidha, Dkt. Jafo, ameongeza kuwa hakuna Nchi yeyote itakayoweza kufanikiwa kiuchumi kama haina Amani, hivyo amewataka watanzania kudumisha Upeno na Mshikamano hasa kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Sambamba na hayo, Mhe. Jafo ameongeza kuwa, changamoto zote zilizotolewa hapo ni mtambuka hivyo kila Waziri mwenye dhamana atapelekewa eneo lake ili zifanyiwe kazi, kwakuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inataka watanzania waweze kukua kiuchumi.

Kwa Upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka, amesema kuwa wakazi wa mkoa wa Njombe ni wachapakazi, kutokana na kuwepo kwa rasilimali nyingi, ambapo amemhakikishia Waziri Jafo kuwa, mkoa huo unazidi kubadirika kiuchumi kadri siku zinavyoenda.  

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Samwel Sweda, amesema kuwa wamepokea maagizo, kwamba mazingira yote ya uwekezaji yameandaliwa vizuri, na uchumi wa wananjombe utakuwa kwa nguvu kupitia sekta ya Kilimo na vyanzo vingine.

Ikumbukwe kuwa, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Seleman Said Jafo, amekuwa na ziara ya kikazi mkoani Njombe, tangu Februari 17, 2025 akianzia wilaya ya Ludewa, ambapo leo kabla ya kumalizia Wanging’ombe na Makambako, amekutana na Wadau wa Sekta ya Uwekezaji na Biashara, Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Mkoa na Halmashauri ili kujadili changamoto na kuzitafutia ufumbuzi.

Matangazo

  • MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 August 15, 2024
  • TANGAZO LA KUSUDIO LA KUTUNGA SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YA MWAKA 2025 January 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED MWAGA KAGUA UJENZI WA MATUNDU ISHIRINI YA VYOO SHULE YA MSINGI MAFIGA

    August 26, 2025
  • DED MAKETE AKAGUA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MEKETE

    August 13, 2025
  • DED MAKETE DC AKABIDHI BENDERA KWA WASHIRIKI WA SHIMISEMITA 2025 - TANGA

    August 13, 2025
  • DED MWAGA ASISITIZA UBORA WA MEJNGO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

Naibu Waziri wa elimu akiwa chuo cha ualimu Tandala
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • TAARIFA KUHUSU MAPATO (LGRCIS)
  • PLANREP
  • MAKETE DC Online TV
  • BEMIS
  • HIMS
  • MAKETE DC Facebook page
  • FFARS
  • MAKETE DC Instagram page

Kurasa Mashuhuri

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • CHF-IMIS DEV
  • Baraza la Mitihani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MAKETE DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la barua: P.O.BOX. 6 Makete, Njombe Tanzania

    simu: +255 262 740016

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@maketedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MAKETEDC . All rights reserved.